Maombi

Baba katika jina la Yesu tunakuomba uibariki Afrika pamoja na viongozi wote wa bara hili. Amani yako ipitayo fahamu za mwanadamu, iitawale Afrika. Hekima yako zaidi ya ile uliyombariki nayo Suleimani mtumishi wako, uimwage Afrika.

Ili watu wako wanaokaa katika bara hili wakagundue hazina iliyofichwa ndani ya fahamu zao,wakaweze kuzitumia bongo zao ili kila wanachokiitaji katika maisha haya ya hapa duniani, waweze kukigundua hapa Afrika.

Vijana wa Bara hili uwabariki ee Bwana. Wape kujua kwamba hawakuzaliwa Afrika kwa bahati mbaya, ila kwa mpango na makusudi yako kamili. Wafungue macho yao ya kiroho waone uzuri uliyo katika bara hili, ili waache kutamani mila natamaduni za nchi za magharibi.

Wanawake wa Afrika waangazie mwanga wako wajue kwamba uliwaumba Wanawake na watabaki Wanawake. Kwa Yesu Kristo.Amina.

<<Back  |  Home |  Gazeti La Injili | Injili1 | Nyimbo Za Munishi | Next >>