Mauaji ya kisiasa Tanzania Marekani ilihusika. |
Polisi nchini Tanzania wamewaua kwa kuwapiga risasi wafuasi zaidi ya 280 wa chama maarufu cha upinzani CUF. Kosa lao inadaiwa kuwa walishiriki katika maandamano ya kudai kurudiwa kwa uchaguzi ambao chama tawala kikisaidiwa na Marekani kiliwanyanganya ushindi wao. Siyo nia yetu kuwalaumu watu ovyo ovyo, lakini uchunguzi wa kisiasa unaonyesha kuwa Marekani ilihusika moja kwa moja katika kusababisha utata huu ambao usipoangaliwa unaweza kuitumbukiza Tanzania katika vita ya wenyewe kwa wenyewe ambayo itakuwa vigumu kuimaliza. Hakuna uchaguzi unaofanyika popote Afrika bila kuingiliwa na Marekani, na uchaguzi uliopita Tanzania Marekani ilikuwepo kwa nguvu zote kulinda maslahi yao. Kile wanachokiita demokrasia, maana yake halisi ni kulinda maslahi yao, na siyo kama wanavyotaka tuamini. Ndiyo maana baada ya kuwa na mkutano na Mkapa, Marekani ilikubali kumsaidia ili ashinde uchaguzi kwa masharti kuwa dhahabu yote ya Tanzania itapelekwa Marekani. Muhimu zaidi katika makubaliano hayo ilikuwa kwamba Mkapa ahakikishe kuwa Zanzibari haitatumiwa na maghaidi wa kiarabu kushambulia balozi za Marekani zilizoko Afrika mashariki na kati kama ilivyofanyika Nairobi na Dar. Baada ya Mkapa kukubaliana na masharti hayo yote, ndipo Marekani nayo kwa upande wake ikamhakikishia kuwa asiwe na wasi wasi kwani itatumia kila mbinu kumrudisha madarakani. Kwa hiyo CCM iliingia kwenye uchaguzi ikijua kuwa lazima itarudi madarakani, lakini ilisahau kuwa wananchi wamechoka nayo na hawaitaki tena. Pamoja na kutumia pesa nyingi kusambaza 'Tshirts' pamoja na picha za Mkapa nchi nzima, bado hiyo haikubadilisha msimamo wa wananchi kuwa CCM imezeeka na sera zake ni mbovu na hawaitaki tena. Lakini CCM wakitumia nguvu zote za dola, walihakikisha kuwa wamerudi madarakani kwa mabavu. Na sasa wana kibarua cha kuwanyamazisha wananchi ambao hawakurithika na jinsi uchaguzi ulivyoendeshwa kana kwamba Tanzania ni nchi ya chama kimoja. Mauaji ya wana CUF 280 yaliyofanywa na Polisi ni ushahidi wa kutosha kuwa Mkapa alijua kile alichokuwa akikifanya. Kwanza mauaji hayo yalifanywa kweupe bila kuogopa 'Camera' za vyombo vya kimataifa, na hii ilikuwa ni kwa sababu ya kuungwa mkono na Marekani ambayo baada ya mauaji hayo ilijikomba kwa kusema inatoa onyo yasirudiwe tena. Onyo lao lilikuwa rahisi kiasi cha kumfanya mtu yeyote mwenye akili timamu ajiulize. Hawa kweli ndio wale wanaohubiri demokrasia duniani au ni wengine? Lakini jibu lilikuwa rahisi. Hakuna demokrasia bila kulinda kwanza maslahi ya Marekani, na ikiwezekana maslahi hayo yalindwe kwa kuwaua watanzania 280 wasio na hatia. Siungi mkono ughaidi unaofanywa na yeyote duniani,lakini sikubaliani na Marekani kwamba kila mwarabu na kila mwislamu ni ghaidi. Mkapa anaweza kushupaza shingo kwa sababu ya kukingiwa kifua na Amerika, lakini asijue kuwa wakati wowote Amerika inaweza kumwacha kwenye mataa. Jambo moja ninalolijua na hawa jamaa wanaotaka kuitawala dunia ni kwamba, wakijua kuwa kiongozi hana kibali kwa watu, wanaachana naye. Na mambo yanavyoonekana ndivyo watakavyofanya kwa Mkapa. Mimi ni Mkristo, lakini kitendo cha Serikali ya Mkapa kuwaua waislamu 280 kimenipa uchungu mkubwa kiasi kwamba machozi yananitoka ninavyooandika makala haya. Lakini niseme nini? Tusubiri tuone mwisho wake. Munishi. |