Anzisheni Redio za Injili: Wito
|
Redio ni nyenzo muhimu ya kuhubiria injili ya Yesu mwokozi. makanisa yakiitumia vizuri inaweza kuwarahisishia kazi yao. Kwa hiyo ni muhimu kwa makanisa kutilia maanani matumizi ya redio kama chombo cha kuipeleka habari njema kwa watu wote. Na itakuwa rahisi zaidi ikiwa makanisa husika yatamiliki redio zao ili kuokoa gharama. Nayapongeza makanisa ambayo tayari yameuona umuhimu huo, na yanaendesha vipindi vya kiinjili katika redio za kibiashara zilizopo. Ni muhimu kuanzisha redio za injili ili kuzitumia kuhubiri habari njema. Dunia inabadilika haraka na kanisa lisipokwenda na wakati litaachwa mbali kimawasilino. Pamoja na kuanzisha redio ni muhimu kujua kutumia vyombo vya mawasiliano kwa ujumla kuepuka makosa yanayofanywa na wahubiri wa TV. na redio. Wanatumia vipaza sauti, na bado wanapayuka kwa sauti ya juu kiasi cha kuharimu makoo yao na masikio ya wasikilizaji wao.Umewahi kumsikia Lai , Mark Kariuki na Muiru? Utajaza mwenyewe. |