|
Kama ulikuwa umedanganyika kuwa Julias Nyerere alikuwa Mkristo, sikia alivyosema."Chama na serikali havina dini," Kwa hiyo Mungu hakuhusishwa katika masuala ya chama na serikali. Hebu sikia Kambarage akisema kwamba, "Tanzania inaheshimu uhuru wa watu wake kuabudu dini yeyote lakini nchi haina dini, ila chama kimeshika hatamu zote."Yaani huwezi kupiga kura au kufanya chochote mpaka uwe mwanachama wa CCM. Uliwahi kumsikia aliposema: Tukimpata rais ambaye hamwamini Mungu wa kweli, tutamwapisha kwa huyo mungu wake. lakini lazima aape kuilinda katiba ya CCM." Hiyo ina maana Nyerere hakumwamini Mungu wa kweli bali alijitukuza kama Mungu. Naona bado una mashaka labda ni kwa sababu hukumsika akisema:"Siasa yetu ni ya ujamaa na kujitegemea wenyewe bila Mungu."lazima watanzania wafanye kazi kwa bidii kwani uti wa mgongo wa Tanzania. Yanasikika kama maneno mazuri. Lakini kwa sababu hayamhusishi Mungu yanabaki kuwa maneno ya kipumbavu kama neno la Mungu linavyosema "Mpumbavu amesema moyoni wake hakuna Mungu."Niseme nini? Maana ni mengi yaliyosemwa na Nyerere kuthibitisha kuwa alikuwa mkoministi asiyeamini kuwa kuna Mungu muumbaji wa vitu vyote anayestahili kuabudiwa na kusifiwa. Ndio maana siasa ya ujamaa ilishindwa vibaya ili ajue kuwa hakuna linalowezekana bila Mungu kuliwezesha. Na kama mungu wa CCM alikufa, na yenyewe itakufa tu waache kutapatapa. |