Kweli hali yetu ni ya kuaibisha |
Kweli hali yetu ni ya kuaibisha na ni sisi wenyewe ndiyo tuliosababisha. Lililopo sasa ni kujitahidi kutofumbia macho uozo wowote unaojitokeza. Kichekesho kimoja kilichojitokeza wiki iliyopita ni pale watu wanne walipoamua kuandamana hadi Hoteli ya Sheraton, ambako wakuu hao wa nchi za mashariki na kusini mwa afrika walikuwa wakikutana na ujumbe wa Benki ya dunia. Amini usiamini! Polisi wetu waliwakamata watu hao na kuwatia msukosuko na hatimae kuwaachia kwa dhamana. Wakati ambapo Rais baadae aliutangazia umma kuutambua uhuru wa waandamanaji hao kujieleza, na kwamba alitegemea suala la watu hao lingekuwa limekwisha, Polisi wetu hadi leo "Wamelishikia bango" suala hilo kwa kisingio cha "uchunguzi unendelea" "enewei" tuishie hapo kwa leo Nategemea michapo zaidi kutoka kwako Sammi. sammituni@hotmail.com |