Nyufa ndani ya CCM zitaigharimu kujenga ukuta safari hii:
Kuna tetesi kuwa mambo ndani ya CCM siyo mazuri kama wengi wanavyofikiria.

Mwaka mmoja tu tangu afariki yule ambaye CCM ilikuwa ikiimba zidumu fikra zake, sasa kuna uhaba wa fikra. Na baadhi ya viongozi wa CCM wanaona siyo vyema kuongozwa na fikra za mtu aliye kaburini.

Hawa ni wale ambao mara nyingi walikuwa hawakubaliani na mawazo ya Nyerere na walikuwa wanaogopa kusema.

Habari tulizozipata kutoka vianzio vyetu ndani ya chama tawala zinasema kuwa hata mweyekiti wa sasa bwana Mkapa, anapata kazi kubwa kuwatiisha viongozi ndani ya chama alichoachiwa kwani wengi hawampi utii waliokuwa wakimpa mwalimu wakati wa uhai wake.

Wengi wanasema ndio sababu kila mara akionekana hadharani huonekana akiwa na jazba au hasira kali. Hii ni kutokana na mambo ndani ya chama, pamoja na vyombo vyote vya dola ukianzia jeshi la polisi na majeshi yote inadaiwa kuwa hayampi utii waliokuwa wakimpa Mwalimu.

Nafasi hiyo ya nyufa ndani ya CCM wapinzani wakiitumia vizuri, wanaweza kuisababisha CCM ijenge ukuta safari hii. Lakini kama hawatapiga mahesabu yao sawasawa, watajikuta pale walipokuwa mwaka 1995.

Ila matumaini makubwa yako kwa kijana chipukizi mwenye sauti kama chiriku, Mwinjilisti Faustin Munishi na ambaye ametangaza kuwa Mungu amemwita aiongoze Tanzania. Itawategemea watanzania kama wataamua kumpa nafasi kijana huyo.

Hekima yake inafananishwa na ile Mfalme Suleiman iliyotoka kwa Mungu na siyo ya elimu ya wanadamu ambao mara nyingi hutoa rushwa wapate vyeti ambavyo hawakuhitimu kuwa navyo. Alizaliwa huko Moshi vijijini katika mtaa wa Kindi chini Muyuni mwaka 1960, alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi Kindi juu mpaka mwaka 1974 alipomaliza darasa la saba. Hakuchaguliwa kwenda sekondari kutokana na kile alichokiita uonevu. Mwalimu mkuu ambaye alipokea rushwa kutoka kwa wazazi ambao watoto wao hawakufanya vizuri miaka ya nyuma, aliwaruhusu kurudia darasa lao na kuwaletea ushindani usio wa kawaida. Munishi ambaye kuanzia darasa la kwanza alikuwa akingangania namba moja mbili au tatu, alijikuta akiwa namba 14 baada ya hao wazee wenye ndevu kuingizwa darasani kwao kupitia mlango wa nyuma. Hiyo haikumkatisha tamaa kijana huyo ambaye tangu wakati huo amekuwa akijitafutia elimu kwa njia yeyote ile aliyoiona inafaa, na kwa sasa inasadikiwa ana elimu zaidi ya Dr. au Profesa yeyote aliyefuzu chuo kikuu chochote duniani. Na kwa kuwa hakuna aliyemtahini elimu ya Munishi inabaki kuwa kitendawili kinachotegulia na yale anayoyaandika kuyasema na kuyaimba, zaidi sana yale anayoyatenda. Vyombo vya habari vimemwita mtu aliyejaliwa kipaji cha ajabu kutoka kwa Mungu. Ni kipaji hicho ndicho tunataka watanzania wasikikose. Watanzania mpeni nafasi Mungu kwa kumchagua Faustin Munishi kuwa kiongozi wanu na tutayaona mabadiliko makubwa katika nchi yetu. Tangu uhuru Tanzania imekuwa ikiongozwa na CCM dini ya mungu Nyerere, ikaharibu nchi, sasa tunataka iongozwe na amri kumi za Mungu wa kweli, na nchi itapona na kubarikiwa.

<<back      Home   Gazeti La Injili    Injili3   Next>>