Mitumba na viwanda

Munishi akiongea moja kwa moja na Radio mpya ya Nation FM leo mchana alikuwa na haya ya kusema. Mitumba ni chochote kilichotumika na badala ya kutupwa kinauzwa ili wale wasioweza kununua vitu vipya wanunue , na hiyo ni popote duniani siyo Kenya peke yake.

Na ukweli wa mambo ni kwamba bidhaa zilizotumika haziwezi kumalizwa duniani.

Lakini wale wanaotetea viwanda vyetu wana haki ya kufanya hivyo, ila utatuzi wa tatizo hilo siyo tu kuzuia biashara ya mitumba ila kuvipatia viwanda vyetu mazingara mazuri ya kuweza kushindana katika soko huru.

Ili kuhakikisha kuwa kuna uwiano wa kibiashara unaofuata sheria ili wengine wasivunje sheria kuwamaliza wengine.

Umasikini usitumiwe kama chambo, kuwaruhusu watu wenye tamaa kuvunja sheria na kufumbiwa macho kwa sababu tu wanauza bidhaa zao kwa bei rahisi.

Sheria zote za usawa wa kibiashara zifuatwe kikamilifu jambo ambalo litawapa wafanyibiashara wote uwanja wa ushindani wa haki kibiashara .

Kwa sasa viwanda vyetu vinapambana na ushindani usiyo haki wa kuvifanya vishindane na viwanda vya nchi za magharibi jambo ambalo kila mtu anajua nani atakayeshindwa.

Kwa hiyo masuala yote ya soko huru na ubinafsishaji wa viwanda usipoangaliwa vizuri, viwanda vyetu vitakuwa vikilia siku zote.

Imeandikwa na Faustin S. Munishi

<<Back  |  Home |  Gazeti La Injili | Injili2 | Nyimbo Za Munishi | Next >>